Search This Blog

Tuesday, October 1, 2013

JE, WAZIJUA FAIDA ZA UKWAJU ?

Ukwaju


Ukwaju ni  moja ya aina ya matunda yapatikanayo hasa mkoa wa Tabora Tanzania na sehemu nyinginezo nyingi Duniani. ngoja tuone faida za ukwaju katika mwili wa binadamu

Basi hizi ni faida za ukwaju ambazo zitakushawishi siku nyingine kuagiza glasi ya juisi ya ukwaju, na kama ni 'waziri wa mambo ya ndani' ya nyumba, au una fahamiana na 'waziri husika' basi agiza aendapo gulioni asiache kuchukua fungu la ukwaju wa kutosha walao wiki kama si mwezi mzima.

  1. Chanzo kizuri cha viuasumu mwilini 'antioxidants' ambavyo huzuia Saratani (cancer)
  2. Chanzo cha Vitamini B na C vile vile "carotentes"
  3. Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya malaria na homa ya matumbo
  4. Huulinda mwili dhidi ya mafua na kero za mafua kooni
  5. Husaidia myeyusho na mmengenyo wa chakula na kuondosha kuvimbiwa
  6. Husaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile disorders)
  7. Husaidia kurahisisha choo (laxative)
  8. Husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na hivyo kuimarisha moyo
  9. Husaidia ngozi kuwa nyororo, vile vile husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua au yenye vidonda
  10. Husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo)


KAZI AU UMUHIMU WA CHUNGWA KATIKA KUKUPATIA MUONEKANO MZURI WA NGOZI YA USO WAKO.

CHUNGWA


Hili ni chungwa maarufu sana linalosaidia kurudishia ngozi iliyodhurika na kuupa uhalisia wa ngozi yako. Jinsi ya kutumia ni rahisi sana, chukua juisi ya chungwa ya baridi kisha paka usoni, acha kwa dakika 10 kisha osha utaona matokeo yake.

KAZI AU UMUHIMU WA NDIZI KUKUPATIA MUONEKANO MZURI WA NGOZI YA MWILI WAKO.


NDIZI: 

NDIZI

Hili ni tunda lenye jina kubwa kwa watu wengi wanaojali ulaji wa matunda, kwani nitamu na lenye ladha safi.Tunda hili husaidia kulainisha ngozi ya uso iliyokauka, kwa mfano utakuta kuna baadhi ya mafuta au losheni zimecholwa ndizi.Kula ndizi ili urekebishe ngozi ya uso wako pamoja na kuupa uwezo mzuri wa  ukumeng'enya chakula. 
jitahidi kupata ndizi kwa muonekano wako mzuri wa ngozi yako

KAZI YA PAPAI KATIKA KUKUPATIA MUONEKANO MZURI WA NGOZI YA MWILI WAKO

PAPAI

PAPAI

Ni tunda sahihi kabisa katika kukupa ngozi yenye mafuta, kurudishia au kuziba sehemu zilizoumia na kunyofoka katika ngozi yako. Papai  pia hunga'arisha rangi ya ngozi yako, yote haya hufanyika na enzyme inayotokana papai ambayo huitwa papain. Endapo kama unataka kutumia papai katika ngozi yako ya uso, basi chukua asali changanya na papai lililo iva na paka usoni kwako kwa dakika 10 kisha safisha, kisha utaona kitakachotokea katika uso wako, utaonekana kama ngozi ya mtoto wa siku mbili.