Search This Blog

Monday, July 1, 2013

Usafi Tanzania Unawezekana

yaliyojili jijini hasa katika Manispaa za Jiji la Dar es Salaam, kama Ilala na Kinondoni zilivyoweza kulisafisha jiji na kuwa safi kiasi cha kuvutia. inadaiwa kuwa kumbe jiji kuwa chafu ni uamuzi wa wahusika wenyewe na si wakazi wake kwani wahusika hao wameweza kuingia mitaani na kufanya usafi kwa zana zilezile za siku zote kulifanya jiji hilo kuwa safi kuliko siku za nyuma na kupelekea jiji hilo ku ng'aa  isivyo kawaiada
da chezea obama wewe

ujio wa Obama Tanzania


RAIS Barack Hussein Obama wa Marekani anaanza ziara ya siku mbili nchini Tanzania leo akitokea Afrika Kusini kwenye mfululizo wa ziara zake barani Afrika akianzia Senegal, Ijumaa Wikienda linakuhabarisha kilichopo nyuma ya ziara hiyo.



yadaiwa kuwa TANZANIA NDIYO NCHI BORA AFRIKA
Mbali na Kikwete kupokea marais wawili wa Marekani, lakini Tanzania inaonekana ndiyo nchi bora zaidi barani Afrika kwa vile ndiyo pekee iliyotembelewa na marais wengi kutoka Marekani.
Mwaka 1999, William Jefferson ‘Bill’ Clinton (67) akiwa Rais wa 42 wa Marekani alitua nchini kwa ziara ya kiserikali na hivyo kuanzisha mfululizo wa waliomfuatia, Bush na Obama.
Clinton aliwahi kuja tena Bongo baada ya kuachia madaraka, Bush naye anaingia nchini leo akiwa ameongozana na mkewe, Laura ambapo Julai 2 na 3, 2013 anatarajiwa kuhutubia kongamano litakalojadili wajibu wa wake wa marais katika kuinua wanawake duniani. Mke wa Obama, Michelle atahudhuria

yadaiwa magari 150 ya msafara wa ziara ya Rais Barack Obama yamewasili nchini, majina ya mawaziri wa Tanzania yatakayoruhusiwa kumpokea kiongozi huyo kuchujwa na makachero wa FBI.