Search This Blog

Tuesday, October 1, 2013

JE, WAZIJUA FAIDA ZA UKWAJU ?

Ukwaju


Ukwaju ni  moja ya aina ya matunda yapatikanayo hasa mkoa wa Tabora Tanzania na sehemu nyinginezo nyingi Duniani. ngoja tuone faida za ukwaju katika mwili wa binadamu

Basi hizi ni faida za ukwaju ambazo zitakushawishi siku nyingine kuagiza glasi ya juisi ya ukwaju, na kama ni 'waziri wa mambo ya ndani' ya nyumba, au una fahamiana na 'waziri husika' basi agiza aendapo gulioni asiache kuchukua fungu la ukwaju wa kutosha walao wiki kama si mwezi mzima.

  1. Chanzo kizuri cha viuasumu mwilini 'antioxidants' ambavyo huzuia Saratani (cancer)
  2. Chanzo cha Vitamini B na C vile vile "carotentes"
  3. Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya malaria na homa ya matumbo
  4. Huulinda mwili dhidi ya mafua na kero za mafua kooni
  5. Husaidia myeyusho na mmengenyo wa chakula na kuondosha kuvimbiwa
  6. Husaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile disorders)
  7. Husaidia kurahisisha choo (laxative)
  8. Husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na hivyo kuimarisha moyo
  9. Husaidia ngozi kuwa nyororo, vile vile husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua au yenye vidonda
  10. Husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo)


No comments:

Post a Comment