Search This Blog

Saturday, January 26, 2013

Hivi kweli Uzalendo wa shule tulizo soma umepotea au...?


                            Ni changamoto kubwa sana ambazo vizazi vingi vinaipata kutokana na kutokuwepo kwa mawazo mbalimbali juu ya kuifikilia kule tulikotoka na haswa kujikita katika hali ngumu ya mazingira ya elimu miungoni mwa matoto wanao pata elimu. kwa data na uhalisia wa maisha ya ya leo tuna viongozi wengi tu ambao wamesoma shule zinazokabiliwa na mazingira magumu sana, yanayopelekea kupungua kwa mahitaji muhimu ya watoto kupata elimu husika , kwa mfano utakuta wapo vionzozi wa juu ambao wamesoma shule za msingi ambazo sasa ziko kwenye mazingira magumu sana , majengo mabovu yanayoonekana kama magofu, miundombinu hakuna. wakati huo viongozi hao husimama kidete na kujidai wao ni wazalendo ndani ya nchi yao wakati wanashindwa hata kusaidia shule walizo soma na kusahau kuwa zimewaweka pale walipo sasa, kwa mfano shule ya sekondari Malangali iliyoko mkoani Iringa wilayani Mufindi ni moja ya shule ambazo zimekuwa zikifanya vizuri katika kufaulisha wanafunzi wake na kuwaandalia mazingira mazuri ya kwenda vyuo vikuu na hatimaye kuwa viongozi wazuri katika nchi hii lakini bado shule hii inamatatizo kebekebe kama upungufu wa nishati, na huduma muhimu mahali hapo wakati shule hii ni shule yenye wanafunzi wenye mahitaji maalumu.licha ya MALANGALI  kuna shule nyingi sana zimefanikiwa kutoa wasomi wengi sana lakini wasomi hao ni kama vipofu.

                Swali tujiulize, hivi kweli kila aliyesoma  hakuyaona matataizo ya shule yake?  anamwachia nani atatue matatizo hayo, ingali ni wewe muhusika ulipita katika changamoto hizooo?? tuwe na macho tutazame tuliko toka tusiishie kukuna vitambi tu nakufikiria walsha mbalimbali  kwaajiri ya kuburudisha makoo yetu.

No comments:

Post a Comment